Psalms 60:5-12


5 aTuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume,
ili wale uwapendao wapate kuokolewa.
6 bMungu amenena kutoka patakatifu pake:
“Nitaigawa Shekemu kwa ushindi
na kulipima Bonde la Sukothi.
7 cGileadi ni yangu na Manase ni yangu;
Efraimu ni kofia yangu ya chuma,
nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala.
8 dMoabu ni sinia langu la kunawia,
juu ya Edomu natupa kiatu changu;
nashangilia kwa kushindwa kwa Ufilisti.”

9Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome?
Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu?
10 eEe Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi,
na hutoki tena na majeshi yetu?
11 fTuletee msaada dhidi ya adui,
kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu.
12 gKwa msaada wa Mungu tutapata ushindi,
naye atawaponda adui zetu.
Copyright information for SwhNEN